Sunday, 8 November 2009

Ukipigwa au kuachwa baada ya kupima wasiliana na Mama Kikwete

Leo nimekumbuka kupitia mtandao wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inayoongozwa na Mama Salma Kikwete nikakutana na taarifa inayowataka wanawake watakaopigwa na waume zao au kupewa talaka kutokana na kitendo cha kwenda kupima virusi vya Ugonjwa wa UKIMWI wampe taarifa ili aweze kuchukua hatua na kulishughulikia tatizo hilo.

Mama Kikwete alitoa wito huo wakati akiongea na wananchi wa wilaya ya Mbarali katika zoezi la kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya afya katika Hospitali ya wilaya hiyo.

Mama Kikwete amewataka wakina mama wampigie au kutuma ujumbe mfupi ikiwa watapata manyanyaso kutoka kwa waume zao baada ya zoezi la kupima afya kwa kupitia simu yake ya mkononi ambayo ni 0754-294450. Kwa taarifa zaidi tembelea mtandao wa Wama.

0 comments: