Sunday, 8 November 2009

Maisha Club yateketea

MOTO umeteketeza klabu maarufu ya burudani jijini Dar es Salaam iitwayo Maisha Club.

Taarifa zilizopatikana kutoka eneo la tukio zinadai kuwa, moto huo ulianza saa nane mchana na kwamba hadi sasa juhudi za kuuzima zinaendelea.

Klabu hiyo inayomilikiwa na Hellen Sweya iliyopo maeneo ya Oysterbay , jijini Dar es Salaam zamani ilifahamika kwa jina la Mambo Club.

Habari zaidi zinasema inasemekana chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme.

Kamanda wa Polisi, Kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, hata hivyo alisema habari zaidi atazitoa Kamanda wa Polisi, mkoa wa Kinondoni Mark Karunguyeye ambaye yuko eneo la tukio.

Habari: Habari Leo; Picha zaidi: Tembelea http://mrokim.blogspot.com/

0 comments: