
Leo mchana mie na wenyeji wangu pamoja wenyeji wa Cape Town tulitembelea mitaa ya Uswazi au "location" iitwayo Nyanga.

Eneo hili ni Uswazi hasa, Watu wanaishi kwenye nyumba za bati au mbao. Kwa wengi wanaotembelea Afrika Kusini hawapati kufika au kuona mitaa hii ta kati. Mdau kama kawaida alitaka kupata "flavour" ya mitaa hii kati siku ya leo.

Tulienda kwenye sehemu moja maarufu kwa uchomaji wa nyama iitwayo Maphindi.

Eneo hili lina mbwa koko wengi tu wanaoshindia mabaki ya nyama zinazoliwa.

Vinywaji huwekwa mahali popote pale. Hakuna meza wala viti. Muziki hutoka kwenye redio za gari walizokuja nazo wateja.

Wenyeji wa mitaa ya kati wakiwa na mwenyeji wangu Dr Patrick Ngoya (Kulia).

Nyama ikiwa tayari kuliwa na wadau.
3 comments:
Shukrani kwa picha,lakini hii nyama ya mnyama gani? inaonekana ianaendana na Beer ya Kilimanjaro bariiidi.
mmh mdau hapo inaonekena kam mkia mmh nina wasiwasi kama mbwa heheh
Duh! sina usemi kamani hii ni nyama kweli? Najua ni nyama lakini ni ya mnyama gani?
Post a Comment